NOKUBONGA QAMPI amekuwa akifahamika kama “Simba Mama” nchini Afrika Kusini baada ya kumuua mmoja wa wanaume watatu waliombaka binti yake na kuwajeruhi wengine. Alishtakiwa kwa mauaji – lakini baada ya malalamiko ya umma mashtaka yalifutwa, na akaweka juhudi zaidi katika kuhakikisha mwanaye anapona majeraha. Ilikuwa ni usiku wa manane wakati simu ilipomuamsha Nokubonga kutoka usingizini.
Msichana aliyekuwa akimpigia alikuwa kilomita 500 kutoka nyumbani kwake – na akamwambia binti yake, Siphokazi, alikuwa anabakwa na wanaume watatu ambao wote walikuwa wanawafahamu vizuri.
Jibu la kwanza la Nokubonga lilikuwa ni kuwapigia simu polisi, lakini hakuna aliyejibu simu yake. Alifahamu fika kwamba ingechukua muda kufika kijijini kwake, eneo lenye uoto wa kijani kibichi lenye milima ya jimbo la Eastern Cape nchini Afrika Kusini. Alikuwa ndiye mtu pekee ambaye angeweza kumsaidia binti yake.
“Nilikuwa na uoga, lakini nililazimika kwenda kwa sababu alikuwa mwanangu,” alisema. “Nilikuwa nafikiria kwamba nitakapofika pal ,huenda atakuwa amekufa… Kwa sababu aliwafahamu wabakaji wake, na kwa sababu walimfahamu na wakafahamu kuwa anawafahamu, huenda wakafikiria kuwa lazima wamuue ili asiende kuwaripoti.”
Siphokazi alikuwa amewatembelea marafiki zake katika kijiji lakini alikuwa amewaachwa peke yake, amelala wakati walipoondoka nje muda wa saa saba za usiku. Baada ya hapo wanaume watatu ambao walikuwa wakinywa pombe katika nyumba moja walimshambulia.
Nyumba ya Nokubonga iliyoezekwa kwa nyasi ina vyumba viwili, ambako amekuwa akilala, na jiko ambako alichukua kisu.
“Nilikibeba nilipokuwa ninatembea kuelekea mahali pa tukio kwa sababu sikuwa na imani na usalama wangu,” alisema. “Ilikuwa gizana ilibidi nitumie tochi ya simu yangu ili niweze kuangalia njia.”
Alisikia sauti ya binti yake akipiga mayowe alipokuwa akikaribia nyumba alipokuwemo. Alipokuwa akiingia chumbani kwake, mwangaza kutoka kwenye simu yake ulimwezesha kupata picha mbaya ya mwanaye akibakwa.
“Niliogopa … Nikasimama tu mlangoni na nikawauliza wanafanya nini. Walipoona nilikuwa mimi, wakaja na hasira kunifuata, hapo ndipo nilipofikiria kuwa ninahitaji kujilinda, ilikuwa ni hatua ya moja kwa moja,” anasema Nokubonga. Nokubonga alikataa kuongelea kwa kina ni nini kilichofuata.
Jaji katika kesi ya Nokubonga dhidi ya wabakaji alisema inaonyesha kuwa “alikuwa na hisia za hasira sana” alipomuona mmoja wa wanaume akimbaka binti yake, huku wengine wawili wakiwa wamesimama kando huku suruali zao zikiwa kwenye magoti, wakisubiri muda wao ufike.
Judge Mbulelo Jolwana aliendelea kusema kuwa, “Nilimuelewa kwamba hasira zilikuwa zimempanda kupita kiasi. Lakini anachokumbuka leo kuhusu hadithi yake, anakiri kuwa alikuwa na hofu kwake na kwa mwanaye- na sura yake inaonyesha huzuni na machungu.
Ni wazi hata hivyo, kwamba wanaume hao walipomfuata kwa hasira alijilinda kwa kisu – na kwamba aliwadunga kisu walipokuwa wakijaribu kutoroka ambapo hata mmoja wao aliruka kupitia dirishani. Wawili wakajeruhiwa na mmoja akafa hapohapo.
Nokubonga hakubaki pale kuangalia ni kiasi gani washambuliaji waliumi . Alimchukua binti yake katika nyumba ya rafiki yake anayeishi karibu.
Polisi walipofika, Nokubonga alikamatwa na kupelekwa kwenye kituo cha polisi ambako aliwekwa mahabusu, “Nilikuwa ninamfikiria mwanangu,” alisema. “Sikuwa na taarifa zozote kumhusu. Lilikuwa ni tukio la kutisha sana.”
Wakati huohuo Siphokazi alikuwa hospitalini akihofia hali ya mama yake na kufikiria kuwa yuko mahabusu ni jambo lililomsikitisha sana.
Katika kipindi cha miezi 18 baada ya shambulio hilo la ubakaji wameweza walau kuendelea na maisha ya Buhle Tonisethe, wakili aliyemuwakilisha Nokubonga mahakamani, anakumbuka kuwa wote walionekana kukata tamaa alipokutana nao kwa mara ya kwanza baada ya shambulio.
Ni nadra sana kwa Afrika Kusini kwa kesi ya ubakaji kushughulikiwa isipokuwa kutajwa tu kidogo kwenye vyombo vya habari. Huenda hii ikawa ni sehemu ndogo tu ya matukio mengi ya ubakaji nchini humo ambako inakadiriwa kuwa watu 110 hubakwa kwa siku – hali ambayo Rais Cyril Ramaphosa hivi karibuni aliitaja kuwa janga la kitaifa.
Baada ya kesi yake kumalizika, aliamua kufichua siri yake ili kuwapa waathiriwa wengine wa ubakaji ujasili, “Ninaweza kumwambia mtu kuwa hata baada ya shambulio la aina ile kuna maisha, unaweza kwenda tena kjatika jamii. Unaweza bado kuishi maisha yako,”anasema.
Nokubonga pia haonyeshi hasira kama anavyolinganishwa na vyombo vya habari kuwa ana usimba
Ana matumaini kuwa wabakaji wa binti yake wataweza kupata mafanikio mazuri maishani mwao. “Ninatumai kwamba watakapomaliza adhabu yao gerezani watarudi wakiwa watu waliobadilika,” anasema, “kuhadithia tukio na kuwa mfano hai.”
0 Comments