DAVID De Gea mlinda mlango wa Manchester United kwa sasa amabakiza mkataba wa mwaka mmoja ndani ya kikosi hicho hivyo uamuzi ni wa mabosi wake kuamua kumuongezea mkataba ama kumruhusu aondoke.
Mpaka sasa De Gea mwenye umri wa miaka 28 amekuwa kwenye mvutano mkubwa na mabosi zake hao akihitaji kulipwa pesa nyingi zaidi ya wachezaji wengine jambo ambalo limekuwa likileta mkanganyiko ndani ya klabu hiyo.
Imeelezwa kwamba klabu ya Paris Saint German (PSG) imeanza kumvutia kasi mlinda mlango huyo huku ikitenga kiasi cha shilingi bilioni 180 kunasa saini yake.
Pia mlinda mlango huyo amekuwa akiwaniwa na Real Madrid hali ambayo inaongeza ugumu na ushindani wa kuipata saini ya mlinda mlango.
0 Comments