Sintofahamu ndani ya klabu ya Yanga kuhusiana na uchaguzi inawezekana imepata suluhu baada ya Shirikisho la soka nchini Tanzania kuingilia kati uchaguzi huo na kuweka wazi utaratibu nafasi na tarehe ya kufanyika uchaguzi huo.
Katika kikao na Waandishi wa Habari kilichohudhuriwa na pande zote mbili Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa TFF Mchungahela ameweka bayana uchaguzi kufanywa Mei 5 badala ya 28 tarehe iliyokuwa imependekezwa na Bodi ya Wadhamini ya Yanga.
Uchaguzi huo utahusisha nafasi zote za uongozi za klabu hiyo ambapo amefafanua kuwa wagombea waliokuwa wamepitishwa kuwania kujaza nafasi zilizowazi, wataingia moja kwa moja katika kinyan’ganyiro hicho bila kujaza fomu tena
Wagombea hao wataungana na wagombea wengine wakati zoezi la kufanya kampeni litakapoanza. Fomu zinaanza kutolewa kesho Jumanne April 2 Makao Makuu ya klabu ya Yanga
Nafasi zinazowaniwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe nane wa Kamati ya Utendaji. Uchaguzi wa Yanga umekuwa ukiingia katika sura mpya kila siku huku kila mmoja kujiona sahihi tangu uchaguzi ulioshindikana kufanya Januari 13 mwaka huu.
0 Comments