Windows

YANGA YAIPIGA MKWARA MZITO LIPULI FC YA MATOLA, YAPANIA KUINYOOSHA NUSU FAINALI KIBABE

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa Lipuli FC ya Matola isahau habari ya kuwafunga tena kwenye mchezo wao ujao wa kombe la Shirikisho hatua ya nusu fainali.

Lipuli iliifunga Yanga bao 1-0 Uwanja wa Samora kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara hali iliyomuibua Matola na kusema anaitaka tena Yanga ainyooshe FA.

"Tulifungwa licha ya kucheza vizuri kwenye mchezo wetu wa ligi kuu ila bahati haikuwa upande wetu tukafungwa, hatua hii wasifikiri wataweza kutufunga hilo wasahau tunakwenda kwao na mbinu mpya na tunawapiga kwao.

"Tulipiga mashuti sita kwenye lango tulishindwa kufunga, wao shuti moja tu ndio lilizama wavuni hivyo utaona ni namna gani wachezaji wangu walicheza vizuri," amesema Zahera.

Lipuli na Yanga zitamenyana mwezi huu Uwanja wa Samora mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho, mshindi atapenya kucheza fainali ili kumpata mwakilishi wa kimataifa.

Post a Comment

0 Comments