MASTAA wa Taifa Stars akiwemo Fei Toto wa Yanga na Jonas Mkude wa Simba mwaka huu wataota ndoto za ajabu.
Wanakutana na maisha ambayo hawakuwahi kuyafikiria. Caf imetoa dola 260,000(Sh.Mil 598) kama advansi ya maandalizi ya Stars kwa ajili ya fainali za Afcon.
Kwa lugha rahisi ni kwamba wachezaji wa Stars wanaeza kuweka kambi popote Duniani na kama fedha haitoshi wanaruhusiwa kuomba nyongeza.
Lakini mechi zote tatu za awali za Stars kwenye Afcon zitachezwa usiku. Kwa mujibu wa taarifa ya Caf mgawo huo umetolewa kama advansi kwa timu zote zilizofuzu fainali za Afcon inayoanza Juni ambayo Stars haikuwahi kufuzu tangu kina Mkude na Feitoto wazaliwe.
Mgawo huo utakatwa kwenye kiwango itakachoambulia timu husika mpaka mwisho wa mashindano kwani kila nafasi kwenye kundi ina kiwango chake.
Kwa kufuzu tu hatua ya makundi kila timu shiriki ina uhakika wa Sh.Bil 1 lakini timu ikivuka hatua ya mtoano mkwanja unakuwa mnene.
Bingwa wa Afcon msimu huu anabeba Sh.Bilioni 10.3 katika mashindano hayo yanayoanza Juni 21 na kumalizika Julai 19. Stars ipo kundi C na Algeria, Senegal na Kenya.
CHANZO: CHAMPIONI
0 Comments