Windows

YANGA YAWEKA REKODI YA AINA YAKE UWANJA WA UHURU TANGU LIGI KUU BARA KUANZISHWA


Timu ya Yanga imeweka rekodi ya aina yake pengine tangu kuanzishwa kwa Ligi Kuu Bara kuanzishwa hapa nchi kwa kuja na aina ya jezi tofauti tena ikicheza dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Katika mechi hiyo, Yanga ilikuja ikiwa na jezi zingine mpya, jezi ambayo imekuwa ni ya tisa sasa kwa timu hiyo kutoka mitaa ya Twiga, Jangwani kwa msimu huu.

Katika mchezo huo ilioshinda kwa bao 1-0, Yanga ilikuja na jezi aina mpya zenye rangi ya njano na michirizi ya kijani na kuwaSAPRAIZI wanachama na mashabiki wake uwanjani.

Hivi karibuni Kaimu Katibu Mkuu wa timu hiyo, Omar Kaya, aliwahi kunukuliwa akisema kuwa wanabadilisha jezi kwasababu wanaamua kama uongozi na hakuna atakayeweza kuwangia cha kufanya.

Mabadiliko hayo ya jezi yamekuwa yakiwakera baadhi ya mashabiki kutokana na kubadilishwa mara kwa mara na kushindwa kujulikana ni jezi ipi rasmi inayotumika ikiwemo ya nyumbani na ugenini.

Aidha, wapo pia ambao wamekuwa wakipongeza wakieleza kuvutiwa na jezi hizo ambazo Yanga imekuwa ikibadilisha kila wakati.

Post a Comment

0 Comments