Vigogo wa Kenya Gor Mahia walizidisha uongozi wao kwenye ligi kuu nchini Kenya baada ya kuvuna ushindi wa mabao mawili kwa moja didhi ya Ulinzi Stars siku ya jumatatu ugani Afraha mjini Nakuru.
Timu hizi mbili zilikuwa zimetoka sare ya moja kwa moja siku chache zilizopita na Gor ilienda kwenye mechi ikitafuta ushindi ambao ungeweza kuzidisha uongozi wao kwenye jedwali.
Mganda Erisa Ssekisambu aliwapa vigogo hao uongozi mnamo dakika ya kwanza. Ulinzi Stars walipambana hadi dakika ya 76 walipopata bao la kusawazisha kupitia Enosh Ochieng.
Dakika nne kabla ya mchuano kuisha, mchezaji wa zamani wa Ulinzi Stars Samuel Onyango aliipigia Gor bao la ushindi, goli ambalo lilihakikisha mibabe hao wanazidisha uongozi wao katika jedwali hadi alama tisa.
Gor Mahia wanaongoza jedwali kwa alama 58 nao Ulinzi ni wa saba kwa alama 36. Gor Mahia watachuana na KCB siku ya Al Hamisi mjini Kisumu.
0 Comments