

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amewaambia klabu ya Simba hawana uwezo wa kumsajili mshambuliaji wa klabu ya AS Vita Club, Jaen Mark Makusu. Imeelezwa.
Taarifa imeeleza kuwa Zahera amewaeleza Simba kuwa hawatakuwa na uwezo wa kumlipa mchezaji huyo kwani kiwango cha malipo yake wao hawajawahi kukifanya kwa mchezaji yoyote yule.
Ameeleza Makusu amekuwa akilipwa kiasi cha mshahara wa milioni 39 kwa mwezi wakati Simba inatajwa mchezaji anayelipwa fedha ya juu ni Emmanuel Okwi anayepokea milioni 12.
Kauli ya Zahera imekuja kufuatia uwepo wa tetesi kuwa Simba ipo kwenye harakati za kumsajili Makusu ambaye yupo na VIta inayoshuka dimbani Jumamosi ya wiki hii kucheza na Al Ahly kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba imetajwa kutaka saini ya mchezaji huyo ambaye wanaamini atawasaidia zaidi kwenye michezo ya kimataifa na hata Ligi Kuu Bara haswa kuiboresha safu ya ushambuliaji.



0 Comments