Windows

MWAMBA WA LUSAKA AWAPIGIA HESABU KALI WAARABU WA ALGERIA


NYOTA wa timu ya Simba, Claytous Chama amesema akili yake kwa sasa imeelekea kimataifa ambapo wataikabili JS Saoura ya Algeria Jumamosi ya mwezi Machi.

Mchezo huo ambao ni wa marudio kwaLigi ya Mabingwa unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu zote mbili kuzitolea macho pointi tatu, huku JS Saoura wakiwa na hasira ya kulipa kisasi baada ya kupoteza mchezo wao wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa.

"Tunafahamu uzito wa wa mechi yetu ijayo ya Ligi ya Mabingwa mbele ya JS Saoura kwamba tukifanya vizuri tytajiweka kwenye mazingira ya kutinga robo fainali nafasi hiyo hatuwezi kuiahca hivihivi.
"Itakuwa ni mechi ya ushindanikwani wenzetu wapo kwao la nasi tutafanya maajabu kupata matokeo mazuri ambayo yatakuwa msaada mkubwa kwetu,", amesema.
Bao la Chama dhidi ya Nkana dakika za lala salama ziliibeba Simba na kuifanya itinge hatua ya makundi tangu ilipofanya hivyo mwaka 2003 enzi za akina Seleman Matola.

Post a Comment

0 Comments