Windows

ZAHERA ATUA OFISI ZA GLOBAL PUBLISHERS NA KUWATAJA SIMBA


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera jana ametembelea katika ofisi za Global Group zilizopo Sinza Mori, jijini Dar ambapo amefunguka kuwa Simba wana nafasi kubwa ya kupenya kwenye hatua ya robo fainali kutokana na mwenendo wa kikosi hasa baada ya kuwatungua waarabu Al Ahly kwenye mchezo wa marudio bao 1-0.

Simba jana wameanza safari wakiwa na msafara wa wachezaji 20 kuwafuata JS Saoura nchini Algeria mchezo utakaochezwa Machi 9 mwaka huu.

“Naona sasa Simba imekuwa na makali, ina uwezo wa kupenya hatua ya robo fainali ukizingatia wameanza kujijenga kisaikolojia na wana cheza vizuri, endapo watacheza wakiwa ni timu nawaona wanafika hatua ya robo fainali aambapoitawasaidia kuongeza pointi kwaajili ya Taifa la Tanzania,” amesema Zahera.

Simba wanashika nafasi ya pili kwenye kundi D wakiwa na pointi sita, wapinzani wao JS Saoura wapo nafasi ya tatu huku anayeburuza mkia ni AS Vita akiwa na pointi nne na kinara wao ni Al Ahly mwenye pointi saba.

Post a Comment

0 Comments