KOCHA msaidizi wa timu ya Tanzania Prisons, Shaban Kazumba amesema kuwa waamuzi wanapaswa kuwa makini katika maamuzi yao ili kuweka usawa katika matokeo hasa wakati huu wa lala salama kwenye ligi.
Prisons walipoteza mchezo wao wa hivi karibuni kwa kufungwa mabao 2-1 mbele ya Singida United iliyo chini ya Fred Minziro kwa sasa.
"Ubora wa ligi unategemea pia maamuzi ya waamuzi ambao wao ndio watafsiri sheria sasa kama watakuwa wanazipindisha wanafanya mzigo kwa wachezaji na benchi la ufundi kuwa kubwa, kila timu kwa sasa inapambana kutafuta matokeo inapotokea dosari kidogo kwa waamuzi haileti picha nzuri," amesema Kazumba.
Tanzania Prison kwa sasa ipo nafasi ya 17 kwenye msimamo baada ya kucheza michezo 28 ina pointi 32.
0 Comments