Windows

ZAHERA ATOA ASILIMIA HIZI KWA SIMBA CAF


Kocha mkuu wa klabu ya Yanga Mwinyi Zahera ameipa asilimia 60 klabu ya Simba kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Zahera pia ametoa asilimia 40 klabu AS Vita kufuzu robo fainali katika kundi D ambalo lina timu zingine ambazo ni Al Ahly na JS Saoura.

Mkongomani huyo amedai Vita hata akishinda mchezo wake dhidi ya Al Ahly na Simba ikapoteza mbele ya Saoura bado itakuwepo.

Mechi ya mwisho Simba wana nafasi kubwa ya kushinda mchezo wa mwisho na kufuzu robo fainali dhidi ya Vita itakayopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Tayari kikosi cha Simba kipo angani hivi sasa kikielekea Algeria kwa ajili ya mechi na Saoura ukiwa ni mchezo wa pili baada ya ule wa kwanza Simba kushinda mabao 3-1.

Post a Comment

0 Comments