Windows

YANGA YAPANIA KUIMIZA ZAIDI SIMBA KWA SASA, YATOA TAMKO HILI JUU YA MAKOMBE


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa kwa sasa anapigia hesabu kubeba makombe yote mawili ambayo anashiriki kwa kuwa uwezo anao na nafasi ipo.

Yanga kwa sasa wanashiriki michuano ya FA pamoja na Ligi Kuu Bara ambako kote wana nafasi ya kutwaa ubingwa endapo hesabu zao zitakubali.

"Kwa sasa sioni cha kunizuia kupata matokeo, licha ya ugumu ambao ninapitia wachezaji wangu wanacheza kwa juhudi na wanajua kwamba mashabiki wanahitaji matokeo.

"Ili niweze kuwapa shukrani mashabiki nawaambia wapambane wacheze kwa nguvu kupata matokeo, hilo lipo mikononi mwao na wanafanya kitu ambacho kinaonekana hivyo bado tuna safari ya kubeba makombe yote, FA na hili la Ligi Kuu Bara," amesema Zahera.

Yanga inaongoza ligi kwenye msimamo ikiwa na pointi 64 baada ya kucheza michezo 26.

Post a Comment

0 Comments