Windows

AZAM FC WATUMA UJUMBE HUU KWA WAPINZANI WAO JKT TANZANIA


KOCHA wa Azam FC, Idd Cheche amesema kuwa kwa sasa kikosi chake kimeanza kujiandaa kwa ajili ya kuivaa JKT Tanzania mchezo wa ligi utakaopigwa Ijumaa Uwanja wa Chamazi.

Cheche alianza kusimamia kikosi cha Azam FC mara baaada ya kupigwa chini kwa aliyekuwa kocha mkuu, Hans Pluijm na msaidizi wake Juma Mwambusi na ameongoza timu yake kwenye mchezo mmoja wa ligi dhidi ya African Lyon na kubeba pointi tatu.

"Kwa sasa tumeanza maandalizi kuelekea kwenye mchezo wetu dhidi ya JKT Tanzania, natambua ni timu imara na bora kwani tulicheza nayo mzunguko wa kwanza ila hakuna namna tunahitaji pointi tatu ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya ushindani," amesema Cheche.

Azam FC wapo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi baada ya kucheza michezo 26 wamevuna pointi 53 na wapinzani wao JKT wapo nafasi ya 6 wakiwa na pointi 36 baada ya kucheza michezo29.

Post a Comment

0 Comments