Windows

Zahera aeleza sababu za Ajibu kuanzia benchi




KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, ameweka wazi kwamba hakuna tatizo lolote kumuweka benchi nyota wake Ibrahim Ajibu kutokana na namna anavyoiangalia timu pinzani ambayo wanapambana nayo.

Ajibu ambaye ni nahodha wa Yanga, kwa sasa amekuwa akiwekwa nje tofauti na michezo ya mwanzoni mwa ligi.


Ajibu alianzia benchi katika mechi dhidi ya Singida United, Alliance na mechi ya jana dhidi ya KMC.

Zahera ameliambia Championi Jumatatu, kuwa hakuna shida yoyote inapotokea anamuweka nje nahodha huyo kwa sababu anakuwa anajua timu fulani ni wachezaji gani ambao anastahili kuanza nao.

“Wengi wamekuwa wakiuliza kwa nini muda mwingine namuweka nje Ajibu lakini jibu lake ni dogo sana.

“Ukitazama kwenye kikosi changu mara nyingi nafanya mabadiliko ya wachezaji, kuna wengine utawaona mechi hii na wengine mechi ijayo wanapumzika.

“Hiyo inatokana na vile ambavyo ninawaangalia wapinzani wetu. Nikijua timu fulani ipo hivi, hapo ndiyo ninapanga wachezaji kadhaa ndiyo watacheza, kwenye suala hilo ndiyo maana unaona kuna muda Ajibu hachezi, hakuna maana kwamba ni mchezaji mbaya bali ni kutokana na vile ambavyo ninamuangalia mpinzani wangu,” alisema Zahera.

Post a Comment

0 Comments