KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Meky Maxime amesema kuwa amejipanga kubeba pointi tatu mbele ya wapinzani wao Mtibwa Sugar.
Kagera Sugar imecheza michezo 28 mpaka sasa kwenye ligi ikiwa imekusanya pointi 33 mchezo wake unaofuata ni dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa Uwanja wa Kaitaba Marchi 16.
Maxime amesema amekuwa na matokeo mabaya msimu huu hali inayomfanya aongeze umakini kwa kuwapa mafunzo wachezaji wake kutokana na kutoeleweka kwa ligi namna inavyokwenda hasa kwenye msimamo na nafasi.
"Kila mmoja kwa sasa hana uhakika na nafasi ambayo yupo kutokana na pointi ambazo timu imekusanya hivyo kwa yule aliye nafasi ya 10 akipoteza mchezo mmoja na yule aliye nafasi ya chini akishinda atajishtukia yupo ndani ya 10 bora.
"Hivyo ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ni lazima nipambambane kupata matokeo mbele ya Mtibwa Sugar, hali si shwari kwa kikosi changu kwa sasa, ushindani unatakiwa ili kumpata bingwa wa kweli," amesema Maxime.
0 Comments