WAMEKWISHA mapema tu acha nisema hivyo baada ya Uongozi wa Simba kuibuka na kusema kuwa ‘mashushu’ waliowatuma wamerejesha mafaili ya ripoti nzima ilivyo kwa wapinzani wao JS Saoura ambao watacheza nao Jumamosi mchezo wa Ligi ya Mabingwa ukiwa ni mchezo wa marudio.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema ripoti waliyopewa mapema baada kutoka kwa watu waliotangulia awali imewapa mwanga wa kutambua namna ya kwenda kuwakabili wapinzani wao hao.
“Tumepewa ripoti ambayo inaonyesha kwamba mazingira ya kule Algeria kwa muda ambao tutacheza kwa hali ya hewa ni changamoto kwani kuna baridi, sasa hilo limetufanya nasi tujiandae kukabiliana na mazingira hayo, tunakwenda tukiamini kwamba kazi ni kubwa ila kikubwa tunahitaji matokeo,” amesema Manara.
Leo Jioni kikosi kinatarajiwa kuondoka kuelekea nchini Algeria kwa kupitia Dubai kikiwa na msafara wa wachezaji 20 pamoja na benchi la ufundi.
0 Comments