Uongozi wa Yanga umewapelekea burudani ya soka kwa Wanyarukolo baada kupeleka mechi zake za nyumbani kwenye Uwanja wa Samora, Iringa baada ya Uwanja wa Taifa kufungwa.
Uwanja wa Taifa na Uhuru vitafungwa kwaajili ya marekebisho yanayofanywa kwaajili ya Mashindano ya Afcon chini ya miaka 17 yatakayofanyika nchini Aprili.
Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi klabu ya Yanga, Venance Mwamoto alisema amepokea taarifa hizo vizuri na kuwasisitiza mashabiki na wanachama kujisogeza uwanjani timu yao itakapofika.
“Watu wa Songea, Mtwara, Morogoro na Dar, wote tuungane kwa pamoja pindi timu yetu itakapokuwa imeanza kucheza katika uwanja huo,” alisema.
Aliongeza kwamba katika uwanja huo wataanza kwa kucheza michezo miwili ya Kagera Sugar na African Lyon.
Adha ya kuhama uwanja haitowakumba Yanga peke yao kwani hata Simba na African Lyon watahusika kwani wanatumia viwanja hivyo kama viwanja vyao vya nyumbani.
0 Comments