Windows

Kalekwa: Sofapaka haina deni lolote na kocha Melis Medo

Hatuna deni lolote na kocha Melis Medo. Hayo ni matamshi ya rais wa klabu ya Sofapaka ya nchini Kenya Elly Kalekwa ambaye amesema kuwa kocha Medo aliamua kuacha majukumu yake mwenyewe kama kocha wa Sofapaka pasi na kushurutushwa na yeyote kutokana na matokeo yasiyo ya kuridhisha

Aidha anasema wapo tayari kujitetea mahakamani ikiwa kocha huyo atawashitaki kwa kuwa wao walifuata sheria baada ya kocha huyo kuwacha kazi yake na kumlipa pesa ambazo alipaswa kulipwa kutokana na mkataba alokuwa nao

Kocha Medo amelalamika kuwa klabu hiyo haikufuata taratibu kabla hajaacha kazi yake na kuwa atawapeleka mahakamani Sofapaka kutafuta kile amekitaja kuwa ni haki yake.

Kocha huyo kadhalika anasema hakushikwa mkono na uongozi wa Sofapaka na wachezaji wa timu hio hawakumkubali huku akidokeza wapo wenye hata hawakuwa wakihudhuria mazoezi yake jambo analosema ni kama dharau

Kalekwa hata hivyo amepinga madai hayo akisema Mido alizidiwa na majukumu yake na akaamua kubwaga manyaga kwa hiari. Aidha anasema lengo lao kwa sasa ni kulitwaa taji la ligi kuu nchini Kenya –KPL. Kwa sasa Batoto ba Mungu wako katika nafasi ya nne kwenye ligi hiyo alama nne nyuma ya viongozi Bandari .

Mido kwa sasa ni kocha wa Mt Kenya FC awali ikifahamaika kama Nakumat huku timu hiyo ikiwa katika hatari ya kushushwa ngazi. Wapo katika nafasi ya 17 kwa alama 12 .


Post a Comment

0 Comments