BAADA ya danadana za uchanguzi wa Yanga kupigwa kwa muda mrefu, hatimaye Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imetaja tarehe rasmi ya uchaguzi.
Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi ya TFF, Ally Mchungahela amesema leo watakutana na kamati mpya ya uchaguzi ya Yanga kujadili kwa pamoja hatma ya uchaguzi huo.'
Uchaguzi huo awali ilitakiwa ufanyike Januari 13 mwaka huu ukapigwa kalenda kutokana na baadhi ya wanachama kufungua kesi Mahakamani kupinga uchaguzi huo
Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika mwaka huu mapema mwezi Machi tarehe 10 mwaka huu
Mgongano ulikuwa mkubwa kutokana na baadhi ya wanachama kutaka nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti Yusuf Manji iachwe kwa kuwa bado wanamhitaji aendelee kuongoza licha ya kwamba aliandika barua ya kujiuzulu..
0 Comments