FIFA imethibitisha kuwa imepokea rufaa ya Chelsea kupinga adhabu ya kufungiwa kuwasajili wachezaji kwa mwaka mmoja, ijapokuwa haijaamua kama itaisitisha adhabu hiyo kwanza wakati wa mchakato wa kisheria na kuiruhusu klabu hiyo kuwasaini wachezaji katika kipindi cha mapumziko ya msimu.
Chelsea awalà ilisema itapinga marufuku hiyo ya kuwasajili wachezaji wapya hadi 2020 ambayo FIFA iliiwekea kwa kukiuka kanuni za kuwalinda wachezaji wadogo dhidi ya ulanguzi.
Katika kesi kama hizo, FIFA ilikubali kutoitekeleza adhabu hiyo wakati wa kesi hiyo ikiwa mahakamani.
Sera hiyo ilizifanya Barcelona na Real Madrid kuwasaini wachezaji kabla ya adhabu zao kuanza kutekelezwa katika miaka ya karibuni. Kisha Barcelona ikafungiwa kuwasaini wachezaji wapya kwa madirisha mawli ya usajili, na Madrid wakazuiwa kwa dirisha moja.
“Hakuna ratiba kamili ya kufanywa vikao vya kesi hiyo na maamuzi yaliyochukuliwa na kamati ya rufani ya FIFA.” Shirika hilo la kandanda duniani limesema katika taarifa.
0 Comments