Windows

Simba wako Algeria tayari kuvaana na JS Soura

Mabingwa wa kandanda kwenye ligi kuu Tanzania Bara Simba SC imefika salama nchini Algeria ambako imeenda kuchuana na JS Soura mtanange wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao utachezwa Jumamosi ya tarehe 9 Machi 2019 majira ya 4 usiku.

Kikosi chenye majina 20 pamoja na bechi la ufundi kimepitia Dubai kabla ya kuunganisha ndege iliyowapelekea moja kwa moja mpaka Algeria ambako mchezo huo utafanyika, Uwanja ni wa Nyasi bandia.

Simba ambayo inashika nafasi ya tatu kwenye ligi na nafasi pili kwenye ligi ya CAF imeondoka ikiwa na matumaini ya kufanya vizuri baada ya mchezo wa mkondo wa kwanza uliofanyika Dar es Salaam, Simba kuibuka na ushindi wa goli 3-0.

Kwa mujibu wa Meneja wa timu hiyo Patrick Ruyemamu amesema kikosi hicho kitakosa huduma ya mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi ambaye anasumbuliwa na majeruhi aliyoyapata Simba ilipocheza na Azam FC. Mlinzi wa Uganda Jurko Murshid pia hajajumuishwa kwenye kikosi kilichosafiri kwenda Algeria.

Simba itanufaika na kurejea kwa kiraka Erasto Nyoni ambaye amerejea baada ya kukaa nje kwa mda mrefu.

Nafasi ya kufuzu kwenye kundi la Simba liko wazi ambapo Al Ahly ina pointi 7, AS Vital – 6, Simba – 6 na JS Soura – 5, hivyo Simba endapo itashinda katika mchezo wa Jumamosi huku Vita akafungwa moja kwa moja itakuwa imefunzu bila kutazama mchezo wa mwisho wa hapa Dar es Salaam ambapo itacheza na Vita.

Mbali na mchezo wa JS Soura na Simba, siku ya Jumamosi hiyo hiyo AS Vita watakuwa na kibarua cha kuikabili Al Ahly, mtanange utakaochezwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.


Post a Comment

0 Comments