Droo ya hatua ya robo na nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports imefanyika leo ndani ya Studio za Azam TV ambapo mabingwa wa zamani wa kombe hilo Yanga SC wamepangwa kukutana na Alliance FC, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Wakati Yanga ikipelekwa Mwanza, mabingwa wengine wa zamani wa michuano Azam FC wamepelekwa mkoani Kagera ambako itakutana na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba na KMC itacheza na African Lyon.
Kwa upande wa wana fainali wa msimu uliopita timu ya Singida United, wao watasafiri hadi mkoani Iringa kukabiliana na Lipuli FC kwenye hatua hiyo ya robo fainali.
Kwa upande wa nusu fainali, ratiba imekaa kama ifuatavyo:-
Lipuli/Singida United vs Alliance/Yanga.
Kagera Sugar/Azam vs KMC/African Lyon
0 Comments