Windows

SIMBA WAIFUATA JS SAOURA NCHINI ALGERIA NA MATUMAINI KAMA YOOTE


KIKOSI cha Simba leo kimekwea pipa kuwafuata wapinzani wao JS Saoura kikiwa na ripoti kamili ya wapinzani wao ambao wameipata kutoka kwa mashushu waliotangulia huku wachezaji wakiahidi kurejea na zawadi ya ushindi kutoka Algeria.

Mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi, unatarajiwa kuchezwa Jumamosi Machi 9, 2019.

Nyota wa Simba, Meddie Kagere amesema wanatambua ushindani ni mkubwa ila kazi yao ni moja tu kutafuta matokeo Uwanjani ili kujiweka kwenye nafasi nzuri kiushindani.

"Hatuna kazi nyingine zaidi ya kutafuta ushindi, morali ambayo tunayo ni kubwa na kila mchezaji anajua wajibu wake, tunakwenda kwa nidhamu tukitambua wapinzani wetu ni timu bora hivyo ili kujiweka katika nafasi nzuri ujanja wetu utakuwa Uwanjani," amesema Kagere.

Mchezo wa kwanza ambao Simba walikuwa wenyeji walishinda ushindi mnono wa mabao 3-0 hali inayowapa kujiamini kuelekea kwenye mchezo wao wa marudio.

Post a Comment

0 Comments