Timu ya PSG wameingia katika wasiwasi wa kumkosa nyota wake Neymar Jr katika mchezo wao wa klabu bingwa Ulaya dhidi ya Man United kufuatia mchezaji huyo kuumia katika kifundo cha mguu wake wa kulia kwenye mchezo wa jana wa French Cup dhidi ya Strasbourg.
Mchezaji huyo alitoka Uwanjani akiwa na machozi baada ya kupata maumivu hayo katika sehemu ile ile aliyoumia msimu uliopita na kumuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu.
Kocha wa PSG Thomas Tuchel alikuwa mkali akidai kuwa mwamuzi ameshindwa kumlinda mchezaji wake mpaka kusababibisha kuumia, kocha wa Strasbourg Thierry Laurey amesema aina ya uchezaji wa Neymar wa kutoheshimu wapinzani ndio unasababisha kufanyiwa madhambi.
“ Ni aina yake ya uchezaji Kama unacheza kama vile usilalamike kama utachezewa rafu “ alisema kiungo wa Strasbourg Anthony Goncalves.
PSG wataivaa Man United katika mchezo wa kwanza wa raundi ya 16 Bora Februari 12 Old Trafford na tayari wapo katika hatihati ya kumkosa kiungo wao Marco Verratti ambaye aliumia katika kifundo cha mguu wake wikiendi iliyopita.
0 Comments