Mapiramidi hayo ya Bent yaliyo na urefu wa mita 79, yalijengwa kwa nasaba ya nne ya mwanzilishi wa Farao, karibu miaka 2,600 kabla ya Kristo.
Yanachukuliwa kuwa na upekee kwa ajili ya vyumba vyake viwili vya ndani. Wanaakiolojia pia waligundua mkusanyiko wa mawe, udongo na mbao baadhi yake zikiwa na mabaki ya miili ya binadamu pamoja na mabaki ya ukuta wa kale.
Serikali nchini Misri inajaribu kufufua sekta ya utalii ambayo iliyumba kufuatia wimbi la vuguvugu la mapinduzi la mwaka 2011 lililomuondoa madarakani Hosni Mubarak.
0 Comments