KOCHA mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa kilichomshinda kwenye mchezo wake ni ubunifu kwa wachezaji kwani walizidiwa maarifa na wachezaji wa Simba.
Zahera amekubali kupoteza mchezo wake wa leo na kuwaweka kiporo Simba mpaka mwakani ili awatungue mabao mengi zaidi.
"Nimeshindwa kuwafunga Simba kwa kuwa walikuwa bora na wachezaji wake wana akili uwanjani, ila mimi sishangai na wala siwalaumu wachezaji wangu wamecheza kwa juhudi licha ya kufungwa leo.
"Nimewaona Simba wakiwa uwanjani walikuwa wanatafuta bao licha ya kuwadhibiti, bado tuna nafasi ya kufanya vizuri michezo yetu ijayo endapo nitapata wachezaji bora ambao ninawahitaji," amesema Zahera.
Mzunguko wa kwanza Simba akiwa mwenyeji alilazimisha suluhu ila leo akiwa mgeni amemfunga mtani wake Yanga bao 1-0 lililofungwa na Meddie Kagere.
0 Comments