PATRICK Aussems, kocha wa Simba amesema kuwa hana hofu na safu yake ya ushambuliaji licha ya ubutu wanaokumbana nao wakiwa karibu na eneo la hatari.
Washambuliaji wa Simba wakiongozwa na John Bocco ambaye ni nahodha wamekuwa wakishindwa kutumia nafasi za wazi wakiwa eneo la hatari hali inayowafanya washindwe kupata mabao mengi kwenye michezo yao ya hivi karibuni.
Kwenye mchezo wa kimataifa dhidi ya Al Ahly Bocco alikosa zaidi ya nafasi mbili za wazi pia kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Mwadui alikosa nafasi tatu za wazi a kwenye mchezo dhidi ya Yanga licha ya kuingia kwenye box zaidi ya mara saba hakuleta hatari nyingi.
"Kwangu mimi sioni hatari washambuliaji kushindwa kufunga, inatokeoa kwenye mpira ila huwa ninawaambia wanapswa wawe makini, nitayafanyia kazi makosa yao hasa katika michezo yetu inayofuata," amesema.
Jana Simba walishinda bao 1-0 dhidi ya Yanga mchezo wa ligi kuu ambao unawafanya wafikishe pointi 39 na kurejea kwenye nafasi ya tatu.
0 Comments