Hivi karibuni Mkurugenzi wa uwekezaji GSM Injinia Hersi Said alihudhuria hafla ya maadhimisho ya miaka 50 klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini
Baada ya hafla hiyo, Yanga na Kaizer Chiefs zilifungua ukurasa wa ushirikiano katika masuala mbalimbali ya soka
Sasa taarifa mpya ni kuwa Yanga huenda ikamchukua kwa mkopo aliyekuwa kiungo wa Simba James Kotei ambaye sasa anacheza Kaizer Chiefs
Kumekuwa na mazungumzo baina ya Yanga/GSM na Kaizer Chiefs ambayo iko tayari kumuachia nyota huyo aliyeshindwa kutamba katika kikosi cha vinara hao wa ligi kuu ya Afrika Kusini
Kotei alijiunga na Kaizer Chiefs mwezi Julai 2019 akisaini mkataba wa miaka mitatu
Kama kila kitu kitaenda sawa, Kotei anaweza kuwa mchezaji wa Yanga kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa Jumatano
0 Comments