Yanga itaanza mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji katika kipindi cha siku 60
Kulingana na taarifa za ndani, hadi kufikia mwishoni mwa msimu huu, Yanga itakuwa imebadili mfumo wake wa uendeshaji na kuwa kampuni
Tayari kuna kampuni zimeonyesha nia ya kutaka kuwekeza Yanga
Kampuni kutoka Arabuni Etisalat ni moja ya zilizoonyesha nia ya kutaka kuwekeza Yanga
Lakini pamoja na kuwa bado hakuna taarifa rasmi kuhusu GSM, lakini ni dhahiri kampuni hiyo imeanza maandalizi ya kuingia 'mazima' kuwekeza Yanga
Mpaka sasa GSM inafanya maboresho ya kikosi, inalipa mishahara ya wachezaji na juzi imemleta kocha mpya Luc Eymael
Pia wamekuwa wakitoa Tsh Milioni 10 kuwapa motisha wachezaji ili washinde kila mechi ya ligi kuu
Wakiwa moja ya wadhamini wa Yanga, GSM watakuwa na nafasi nzuri zaidi ya kushinda zabuni wakati tenda itakapotangazwa
0 Comments