Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa mlinda lango wa Yanga Ramadhani Kabwili
Kabwili alijiunga na mabingwa hao wa kihistoria miaka mitatu iliyopita wakati huo akiwa na umri wa miaka 16 tu
Msimu huu amekuwa hapati nafasi mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza kutokana na uwepo wa Farouq Shikhalo na Metacha Mnata
Lakini kupitia michuano ya kombe la Mapinduzi, Kabwili amedhihirisha bado yuko vizuri
Yanga ilichukua uamuzi sahihi wa kumuongeza mkataba kwani umri wake bado mdogo
Tunamtakia kila la kheri katika siku hii ya kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa
Bila shaka leo shamrashamra zitakuwa kubwa kambini kwani Kabwili ndiye kinara wa kuwaandalia wachezaji wenzake matukio ya birthday!
HAPPY BIRTHDAY KABWILI..!
0 Comments