KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amesema kuwa malengo yake ya kumaliza akiwa kwenye nne bora bado hayajafa licha ya kupitia kwenye kipindi kigumu.
Katwila amesema kuwa uwezo wa wachezaji wake unaimarika kila siku hali ambayo inamfanya aamini atapata matokeo chanya kwenye michezo yake inayofuata.
"Tuna nafasi kubwa yakupata matokeo na wachezaji wana uwezo mkubwa licha ya mwanzo kupitia changamoto za kawaida zilikuwa zinatukamata ila kwa sasa moto wetu hauzimwi.
"Maandalizi kila baada ya mechi tunafanya ili kuboresha kikosi chetu, lengo letu ni kuona timu inafika kwenye nne bora na kuendelea kutoa ushindani kwa timu nyingine za ligi," amesema Katwila.
Mtibwa Sugar imecheza michezo 26 ipo nafasi ya 8 ikiwa na pointi 35 mchezo wake unaofuatwa ni dhidi ya Stand United Uwaja wa Manungu.
0 Comments