Baada ya kusota benchi kwa muda mrefu hatimaye kiungo wa Simba aliyesajiliwa kutoka Mtibwa, Ibrahim Mohammed, anatarajiwa kusafiri kuelekea Colombia kwa ajili ya majaribio, imeelezwa.
Mo atasafiri kwenda Colombia kufanya majaribio na klabu moja ambayo jina lake bado halijawekwa wazi.
Kiungo huyo amekuwa hana bahati wakati Simba ikinolewa na Kocha Mcameroon, Joseph Omog pamoja na Mbelgiji wa sasa Patrick Aussems pia Mfaransa Pierre Lechantre.
Taarifa imeeleza Mo anaweza kuondoka siku yoyote kuanzia leo ili kujaribu bahati yake ya soka la kimataifa.
Wakati huo kikosi cha Simba kimesafiri kuelekea Algeria kwa ajili ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Saoura itakayopigwa Jumamosi hii.
Simba wanaenda kucheza na Saoura wakiwa na alama 6 kunako kund D na wakiwa wana kumbukumbu ya ushindi wa mabao 3-1 katika mchezo wa kwanza uliopigwa Dar es Salaam.
0 Comments