Windows

MKWAKINYO, MADADA WANANISUMBUA INSTAGRAM


BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo, amefichua kuwa kwa sasa amekuwa akipata meseji nyingi za kutakiwa kimapenzi kutoka kwa wanawake tofauti katika mtandao wa kijamii wa Instagram jambo ambalo halipi nafasi kwake.

Mwakinyo anayedhaminiwa na kampuni ya michezo ya kubashiri nchini ya SportPesa, amekuwa maarufu zaidi kufuatia kuendeleza rekodi yake ya kutoa vipigo baada ya wikiendi iliyopita kumchapa Sergio Gonzalez ‘El Tigre’ TKO ya raundi ya tano kwenye pambano lililofanyika Nairobi, Kenya.

Mwakinyo alisema kuwa amekuwa akipokea jumbe nyingi kutoka kwa wadada mbalimbali ambao wamekuwa wakimtaka kimapenzi jambo ambalo limekuwa likimshangaza kwa kuwa siyo malengo yake.

“Usumbufu umekuwa mkubwa kutoka kwa wadada maana sasa hivi napokea meseji nyingi kupitia mtandao wa Instagram na kila mmoja ananieleza ametokea kunipenda anaomba niwe naye jambo ambalo kwangu wanatakiwa wasahau kabisa kunipata, maana siyo wa hivyo.

“Unajua nilielezwa mapema juu ya huu umaarufu ulivyo jambo ambalo nimelizingatia kwa kuwa nina malengo yangu ambayo sijayafikia halafu licha ya hivyo utanipendaje kwa kuwa tu umeniona katika mtandao!” alisema Mwakinyo.

Post a Comment

0 Comments