Windows

Higuain astaafu kandanda la kimataifa

Mshambuliaji wa Chelsea Gonzalo Higuain ametangaza kustaafu kandanda la kimataifa, akitaja sababu za kifamilia. Higuain mwenye umri wa miaka 31 aliifungia timu ya taifa ya Argentina mabao 31 katika mechi 71. Mechi yake ya mwisho ilikuwa ushindi wa 2 – 1 dhidi ya Nigeria katika Kombe la Dunia Juni mwaka jana nchini Urusi.

Higuain aliiambia televisheni ya Fox Sports: “ muda watu na Argentina umekwisha. Baada ya kuwaza sana nahisi wakati umekwisha. Kwa furaha ya wengi, sasa ntaliangalia tu suala hilo kuoka upande wan je. Nimezungumza na kocha Lionel Scaloni na kumwambia hoja yangu. Nimefanya uamuzi huo kwa sababu nataka kuwa na wakati mzuri na familia yangu. Nataka kuwa na binti yangu, na wakati huo huo nnahisi kuwa nilijitolea sana kwa nchi yangu kwa kufanya chochote kilichowezekana.”

Higuaina mbaye amefunga mabao mattau katika mechi 10 tangu alipojiunga na Chelsea kwa mkopo kutoka Juventus mwezi Januari, aliongeza “Nimeelekeza fikra zangu kikamilifu kwa Chelsea. Ligi ya Premier ni nzuri sana na nnataka kuifurahia. Ina ushindani mkali sana.”


Post a Comment

0 Comments