Windows

Kuelekea mechi na Waarabu-Simba yatabiliwa makubwa,Kocha Pluijm atoa yamoyoni.

. Kocha wa zamani wa Azam FC, Hans van der Pluijm amesema Simba ina nafasi ya kufanya maajabu katika Ligi ya Mbingwa Afrika.

Akizungumza kwa simu jana, Pluijm alisema Simba haipewi nafasi kulinganisha na timu za Kundi D, lakini inaweza kuwashangaza wadau wa soka Afrika

Pluijm ambaye alirejea Ghana juzi, alisema kocha wa Simba Patrick Aussems ni mjanja ana mbinu nzuri za kufundisha soka, pia ana kikosi kipana cha ushindi.

Kocha huyo raia wa Uholanzi alisema ana amini mchezo wa Jumamosi dhidi ya JS Saoura ya Algeria utakuwa mgumu, lakini ana matumaini Simba itapata matokeo mazuri.

“Kama wachezaji watapata maandalizi mazuri ya kimwili na kiakili kujiandaa kwa mchezo huo haitakuwa kazi ngumu Simba kufanya mambo makubwa katika mashindano haya,” alisema Pluijm aliyewahi pia kuzinoa Yanga na Singida United.

Simba itapepetana na JS Saoura ikiwa na mtaji mzuri wa mabao, baada ya kushinda 3-0 yaliyofungwa na Meddie Kagere (mawili) na John Bocco.

Simba inashika nafasi ya pili katika msimamo wa Kundi D ikiwa na pointi sita nyuma ya Al Ahly ya Misri (saba), AS Vita (tano) na JS Saoura (nne).

Chanzo ni Mwanasport.Online


Post a Comment

0 Comments