Kiongozi wa klabu ya Bayern Munioch Karl-Heinz Rummennige amemshutumu vikali kocha wa timu ya Ujerumani Joachim Löw kutoa katika wakati usio muafaka tangazo lake la kuwaondoa Thomas Müller, Jerome Boateng na Mats Hummels kwenye mipango yake ya usoni.
Rummennige amekasirishwa kuwa Löw aliangusha bomu hilo Jumanne – wiki moja kabla ya mchuano muhimu wa Bayern nyumbani dhidi ya Liverpool katika Champions League na pia katikati ya mapambano ya kuwania ubingwa wa Bundesliga.
“Tunazingatia muda na mazingira ya tangazo hilo, kwa wachezaji na umma, kuwa vya kuzusha maswali,” ilisema taarifa ya pamoja ya mwenyekiti wa Bayern Rummennige na mkurugenzi wa spoti Hasan Salihamidzic.
“Mchuano wa mwisho wa kimataifa wa timu ya taifa ya Ujerumani ulichezwa Novemba 19 2018 – miezi mitatu na nusu iliypopita”. Alisemam Rummennige
“2019 ndio mwaka wa mwanzo mpya wa timu ya taifa ya kandanda ya Ujerumani,”Alisema Löw.
“Ilikuwa muhimu kwangu binafsi kufafanua mawazo yangu na mipango yangu kwa wachezaji na mameneja wa FC Bayern.” Aliongeza Löw aliyesafiri hadi Munich kzungumza na wachezaji hao watatu.
Aliyekuwa kiungo wa Bayern na Ujerumani Lothar Mattaeus pia alizusha maswali kuhusu uamuzi huo akisema sio kwamba ni mbaya, bali unasababisha sasa mazingira mabaya katika kikosi cha Bayern mnamo wakati huu muhimu wa msimu.
0 Comments