Kocha Mkuu wa kikosi cha Serengeti Boys, Oscar Mirambo amesema watafanya marekebisho kadhaa licha ya ushindi wa mechi yao ya leo dhidi ya Australia.
Serengeti Boys imeitwanga Australia kwa mabao 3-2 katika mechi ya michuano ya Uefa Assist inayoendelea hapa mjini Antalya.
MIRAMBO (WA KWANZA KUSHOTO) |
Mirambo amesema badala ya mazoezi ya kawaida tu maarufu kama recovery, wanalazimika kufanya mazoezi maalumu kuangalia wanachokosea.
“Bado kuna kitu hakijakaa sawa, hata kama tumeshinda lazima tuyafanyie kazi mambo kadhaa.
“Vijana wanajitahidi lakini kuna mambo wanapaswa kubadili kidogo ili kuweka sawa kile tunachokiamini,” alisema.
Katika mechi ya leo, Serengeti Boys ililazimika kusawazisha mara mbili na pia kufunga bao la ushindi katika dakika ya 89 kupitia Kelvin John.
Mechi ya kwanza, Serengeti Boys ililala kwa bao 1-0 dhidi ya Guinea na ilichezwa wakati wa mvua kubwa.
0 Comments