Kikosi cha Simba leo kinaondoka kuelekea Algeria kwaajili ya Mchezo dhidi ya Js Saoura.
Leo jioni kikosi kitaondoka kuelekea nchini Algeria kwa kupitia Dubai, UAE ambako kitacheza mchezo wa tano wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Saoura, mchezo ambao utachezwa siku ya Jumamosi Machi 9, 2019. Tuikumbuke timu yetu kwenye dua ili ifike salama na ifanye vizuri katika mchezo huo muhimu. #NguvuMoja
0 Comments