KINARA wa kutupia mabao bongo kwa sasa Ligi Kuu Bara, Salim Aiyee wa Mwadui FC ambaye amewakimbiza kwa mbali washambuliaji wote wasumbufu wa kucheka na nyavu ameibuka na kusema kazi bado inaendelea.
Aiyee amemuacha kwa mbali kinara wa msimu uliopita Emmanuel Okwi kwa jumla ya mabao 7 kwani mpaka sasa Okwi amecheka na nyavu mara saba, huku wanaomfuatia ni Heritier Makambo na Meddie Kagere wa Simba wote wana mabao 12.
"Hakuna anayenipa hofu, hapa ni mwendo wa kupambana ili kufikia malengo ambayo nimejiwekea, nashukuru kwa ushirikiano mkubwa ambao napata ndani ya timu ninaamini nitafanya makubwa zaidi.
"Wote ambao tunashindana nao ni kitu cha kawaida kuwa kwenye hali hii ila ni wakati tu unaamua najua wanajua ila ni lazima niwape taabu kidogo hao wanaoitwa kina Makambo na Kagere maana wote tunacheza ndani ya dakika 90," amesema Aiyee.

0 Comments