Windows

Mbwana Samatta acheleweshewa ubingwa KRC Genk




Timu ya nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta, KRC Genk ya Ubelgiji, imechapwa 3-2 na wapinzani wao kwenye mbio za ubingwa, Club Brugge.

Endapo wangeshinda, Genk wangetangazwa mabingwa kwani wangewazidi Brugge kwa pointi 9 ambazo wasingeweza kuzifikia kwa sababu ingekuwa imebaki michezo miwili tu. Genk waliingia kwenye mchezo huu wakiwa na pointi 50, sita juu ya Club Brugge iliyokuwa na pointi 44.

Lakini ushindi wa Brugge una maana kwamba mbio za ubingwa zinaweza kuendelea hadi siku ya mwisho endapo timu hizo mbili zitashinda michezo yao ijayo.

Genk wamebakiza michezo miwili migumu dhidi ya wababe wa soka la Ubelgiji, Anderlecht ambao watacheza nao ugenini Alhamisi ya Mei 16, huku Standard Liège watakaomaliza nao nyumbani Jumapili ya Mei 19 mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments