Windows

Zahera alezea Makambo kubaki Yanga

Zahera alezea Makambo kubaki Yanga

Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera, amesema licha ya mshambuiliaji wa Yanga Heritier Makambo kutajwa kwenye orodha ya wachezaji 40 wa timu ya taifa kuelekea mchezo dhidi ya Liberia lakini anaweza asiondoke nchini.
Zahera ambaye ni kocha msaidizi wa DR Congo, amelifanunua hilo leo kwenye Kipenga Xtra ya East Africa Radio, ambapo ameibainisha kuwa kutajwa kwa mchezaji katika majina 40 haimanishi moja kwa moja ataitwa.
”Unajua huu ni utaratibu wetu kwenye timu ya taifa, tunaita wachezaji 40 ndani ya siku 30 kabla ya mchezo kisha tunawachuja mpaka 23 ndani ya siku 15 kabla ya mchezo hivyo Makambo anaweza kuwa sehemu ya kikosi cha wachezaji 23 au asiwepo”, amesema.

Aidha Zahera amefafanua kuwa wachezaji wote 40 hujulishwa kuwa wawe tayari muda wowote wanaweza kuhitajika kuitumikia timu ya taifa kwahiyo hata Yanga wanayo barua ya wito wa Makambo kwenye timu ya taifa.

DR Congo itashuka dimbani kucheza mechi yao ya mwisho kwenye kundi G kuwania kufuzu fainali za AFCON 2019 dhidi ya Liberia ambayo itapigwa Lubumbashi Machi 22.

Post a Comment

0 Comments