BAADA ya kufanya vizuri katika mechi za Yanga za hivi karibuni, kipa wa timu hiyo, Klaus Kindoki, raia wa DR Congo, amewaambia mashabiki wa timu hiyo kuwa wasubiri mambo makubwa zaidi.
Kindoki hakuwa na mwanzo mzuri ndani ya timu hiyo, hasa baada ya kuruhusu kufungwa mabao matatu katika mechi ya mzunguko wa kwanza mbele ya Stand United, iliyopigwa Uwanja wa Taifa, Dar na Yanga kushinda 4-3.
Kipa huyo hajaruhusu bao kwenye mechi mbili alizocheza hivi karibuni mbele ya Namungo kwenye Kombe la Shirikisho (FA) na Alliance kwenye Ligi Kuu, huku Yanga wakishinda zote.
Kipa huyo aliyetokea Klabu ya Racing de Kinshasa ya kwao DR Congo kabla ya kusaini Yanga, amesema kwa sasa ana furaha baada ya mashabiki wa timu hiyo kumuamini tofauti na mwanzo huku akiahidi kufanya vizuri kuliko ilivyo kwa sasa.
“Nina furaha sana kwa ma shabi k i wa Yanga kunipa muda, ninawaahidi nitawapa furaha zaidi wao kuliko ilivyo kwa sasa,” alisema Kindoki.
Akizungumzia juu ya kiwango cha kipa huyo kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera alisema: “Mimi sijawahi kusajili mchezaji mbaya, watu walikuwa wanasema Kindoki ni mbaya kwa sababu eti anafanya makosa na kufungwa mabao, lakini hawakumbuki kwamba makipa wakubwa wameshafanya makosa na kuzigharimu timu zao.”
0 Comments