Usiku wa March 12 2019 Juventus walikuwa nyumbani kwao Turin kuikaribisha Atletico Madrid katika mchezo wao wa marudiano wa hatua ya 16 bora wa UEFA Champions League msimu wa 2018/2019, Juventus walikuwa wanaingia kucheza mchezo huo wakiwa nyuma kwa magoli 2-0 waliyofungwa katika mchezo wa kwanza.
Mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo akifunga moja ya magoli yake katika mchezo wao dhidi ya Athletico Madrid.
Hivyo kunusuru maisha yao katika michuano hiyo walikuwa wanahitajika kupata ushindi wa kuanzia mabao matatu na kuendelea, hata hivyo licha ya hofu kwa mashabiki wa Juventus kuwa kubwa kuwa wanaweza kulazimishwa sare kutoka Atletico Madrid kutokana na asili ya timu hiyo kuwa na safu nzuri ya ulinzi.
Athletico Madrid walionekana kushindwa kuhimili presha ya Cristiano Ronaldo wa Juventus na kujikuta akiingia wavuni mara tatu kwa kufunga hat-trick, Ronaldo aliifungia Juventus goli la kwanza dakika ya 27, 49 na 86 kwa mkwaju wa penati na kuindoka Atletico kwa kipingo cha magoli 3-0 (Agg 3-2), hivyo ni wazi Juventus imekata tiketi ya kucheza robo fainali ya michuano hiyo.
Wachezaji wa Juventus wakiwa katika vyumba vya kubadilishia nguo baada ya ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Atletico Madrid na kutinga hatua ya robo fainali ligi ya mabingwa Ulaya.
0 Comments