Windows

AZAM FC YATINGA NUSU FAINALI KIBABE, SASA KUKUTANA NA KMC NUSU FAINALI


JOSEPH Mahundi, kiungo mshambuliaji wa Azam FC anaipeleka Azam FC hatua ya nusu fainali ya kombe la Shirikisho baada ya kufunga bao la ushindi dhidi ya Kagera Sugar.

Azam FC wanashind bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar licha ya Kagera kupambana kutafuta matokeo kwenye mchezo wa leo.

Dakika ya 79 Mahundi alipachika bao hilo akimalizia pasi ya Donald Ngoma bao lililodumu mpaka dakika ya 90.

Mlinda mlango Razack Abarola alionyeshwa kadi nyekundu na mwamuzi baada ya kumchezea rafu mchezaji wa Kagera Sugar hali iliyofanya mwalimu Idd Cheche kufanya mabadiliko kwa kumtoa Obrey Chirwa na nafasi yake kuchukuliwa na Mwadin Ally dakika ya 67.

Azam FC sasa itamenyana na KMC ambao wao walitangulia jana baada ya kuibuka kidedea mbele ya African Lyon kwa ushindi wa mabao 2-0.

Post a Comment

0 Comments