Windows

MOURINHO AINYIMA UBINGWA LIVERPOOL


KOCHA Jose Mourinho amesema Liverpool hawana ubavu wa kutwaa ubingwa wa Premier League kwa kuwa kuna vitu wanavikosa.

Kocha huyo Mreno ambaye hana timu kwa sasa baada ya kufukuzwa Manchester United, alihoji utimamu wa upambanaji wa Liverpool inayonolewa na Jurgen Klopp mara baada ya kutoka sare dhidi ya Everton, Jumapili iliyopita.

Mourinho amewataja baadhi ya wachezaji ambao anaona wameshuka ubora kwa miezi ya hivi karibuni, ambao ni James Milner na Roberto Firmino.

"Liverpool hawapo katika ubora waliokuwa nao miezi michache iliyopita, walikuwa wakielekea pazuri. Sasa hivi Salah anakosa nafasi za wazi.

"Wiki sita zilizopita alikuwa na uwezo wa kufunga katika nafasi tofauti, lakini sasa hivi hicho hakipo.

"Milner alikuwa bora lakini sasa hivi amekuwa hata anawekwa benchi kwa kuwa kiwango kimeshuka, ndivyo ilivyo kwa Firmino, walikuwa majeruhi nab ado hawajarejea katika ubora wao," alisema kocha huyo.

Post a Comment

0 Comments