Kuelekea katika mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba utakaopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, kocha wa timu ya Mbao FC, Salum Mayanga ameibuka na kusema kuwa wamefanya mazoezi maalumu ya kuhakikisha wanawazuia washambuliaji hatari wa Simba.
Hiyo ndiyo mechi yake ya kwanza kwa Mayanga kusimamia tangu alipoajiriwa na wababe hao wa Mwanza kwa mkataba hadi mwisho wa msimu huu.
Mayanga alisema kuwa maandalizi yao mpaka sasa yapo vizuri na wanajua kuwa wanaenda kukutana na timu yenye washambuliaji hatari, hivyo amewapa wachezaji wake mazoezi maalumu ya kuhakikisha wanawazuia mastaa hao wa Simba wakiwemo John Bocco na Meddie Kagere.
“Maandalizi yetu mpaka sasa yapo vizuri tumejipanga vya kutosha, tunajua kuwa tunaenda kukutana na timu ya namna gani.
"Kwa hiyo hilo tunalijua na tumefanya maandalizi ya kuhakikisha tunawazuia akina Kagere kwa kuwapa mazoezi maalumu,” alisema Mayanga.
0 Comments