UONGOZI wa Yanga umesema kuwa wachezaji wao wa kikosi cha kwanza wanaingia kambini leo kujiandaa na mchezo wao wa kombe la FA dhidi ya Biashara United utakaochezwa Januari 31 Uwanja wa Taifa.
Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten amesema wanamini watafanya vizuri katika mchezo wao kutokana na maandalizi ambayo walianza kuyafanya baada ya kutolewa kwenye michuano ya SportPesa Cup.
"Biashara United ni kikosi kizuri na ukizingatia kwamba wamefanya mabadiliko ya benchi lao la ufundi ila hilo halitupi taabu tutapambana.
"Leo tunaingia kambini rasmi kwani mwanzo timu ilikuwa inafanya mazoezi na wachezaji wanarejea nyumbani ila kwa sasa tunataka wawe sehemu moja ili kujenga timu vizuri," alisema Ten.
0 Comments