Windows

SIMBA KUWAFUATA WAARABU LEO, WABEBA MATUMAINI YA KUIBUKA WABABE


MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba wanatarajia kuondoka leo wakiwa wamebeba matumaini ya kupata matokeo mbele ya wapinzani wao Al Ahly ya Misri kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa hatua ya Makundi utakaochezwa Februari 2.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema msafara wa klabu utakuwa na wachezaji 20 pamoja na baadhi ya Viongozi utaondoka leo jioni kwa kupitia Addis Ababa nchini Ethiopia kisha kuelekea Mjini Alexandria nchini Misri.

"Tunawaheshimu wapinzani wetu na tunatambua kuwa mchezo utakuwa mgumu, wachezaji wanatambua nafasi hii ni kwa ajili ya kuturejeshea furaha wana Simba, nina amini kwenye mpira chochote kinaweza kutokea," alisema Manara.

Kwenye kundi D Al Ahly wanaongoza wakiwa na pointi nne huku Simba wakiwa nafasi ya tatu baada ya kukusanya pointi tatu katika mchezo wao wa kwanza mbele ya JS Saura ya Algeria. 

Post a Comment

0 Comments