Windows

MTIBWA SUGAR WAFUNGUKA KILICHOWAPONZA WAPINZANI WAO FA


KOCHA wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amesema kilichowasaidia kuibuka na ushindi jana mbele ya Majimaji Uwanja wa Manungu ni uzoefu wa wachezaji wake pamoja na kujituma ndani ya Uwanja.

Mtibwa jana waliibuka wababe katika mchezo wa raundi ya nne michuano ya FA uliochezwa Uwanja wa Manungu kwa ushindi wa mabao 2-1.

"Bao la mapema dakika ya nne lililofungwa na Riphat Khamis lilitufanya tuwe na nguvu ila nao waliposawazisha dakika ya saba kupitia kwa Antony Mwingila walianza  kucheza kwa kasi na kujiamini hali ambayo iliwaponza.

"Niliwaambia wachezaji watulie wanaweza kupata ushindi na ndicho kilichotokea tukapata ushidi nyumbani wa mabao 2-1 na yote yakifungwa na Khamis," alisema Katwila.

Mtibwa Sugar ni bingwa mtetezi wa michuano hii alipata nafasi ya kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa mwaka jana ameingia kwenye hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.


Post a Comment

0 Comments